November 29, 2018



Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya Yanga na JKT Tanzania ambayo ilitakiwa ichezwe leo saa 12:00 jioni itachezwa saa 10:00.

Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa wamelazimika kurudisha nyuma muda wa mechi hiyo pamoja na mechi nyingine zinazofuata kutokana na mmiliki wa uwanja huo kutoa taarifa za kutowasha taa.

"Mmiliki wa uwanja wa Taifa amesitisha zoezi la kuwasha taa usiku kwa mechi ambazo zitachezwa uwanja wa taifa, ambazo zingehitajika, hivyo mechi zote zitachezwa majira ya 10:00 Jioni," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic