MABOSI SIMBA WAPEWA MAJINA HAYA MAWILI
Hatimaye mabosi wapya wa Simba wamekabidhiwa majina mawili ya wachezaji wanaotakiwa na Mbelgiji Patrick Aussems kwenye dirisha hili la usajili.
Dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa Novemba 15 yaani kesho kwa timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara na zile za Ligi Daraja la Kwanza.
Simba ambayo ilifanya uchaguzi wake hivi karibuni na Swedy Mkwabi kuwa Mwenyekiti, juzi ilifanya kikao cha kwanza cha bodi ambapo moja ya mambo yaliyojadiliwa ni usajili wa dirisha dogo na mapendekezo ya kocha wao.
“Tumejadili mambo mengi lakini ukweli ni kwamba tulielezwa pia juu ya usajili ambapo kocha amependekeza kusajili wachezaji kwenye nafasi mbili tu, ambapo anamtaka beki wa kulia na kiungo mkabaji tu.
“Hawa ndiyo wachezaji ambao tumekabidhiwa kuwa kocha anawataka, na sisi kazi yetu ni kusajili ili timu iwe bora.
“Unajua sisi nafasi zote alizosema kocha hatuna mbadala, Shomari Kapombe akiwa hayupo basi kule kwake kunakuwa na tatizo, lakini pia kiungo mkabaji wetu ni Jonas Mkude, akikosekana pale panayumba hivyo lazima tuhakikishe tunafanya jambo ili kuepuka hilo,” kilisema chanzo cha ndani cha uhakika.
kWA MANTIKI HIO kAHATA HANA NAFASI SIMBA MAANA YULE NI KIUNGO MCHEZESHAJI TENA WA DIMBA LA JUU, LABDO KOCHA AMBADILI, LAKINI SIMBA WANATAKIWA WAPATE MTU WABOX TO BOX MIDFIELDER KAMA ALIVYO CONTE, TEROIRA, BUSQOUTE, VIDAL, CASEMIRO ..................
ReplyDelete