November 28, 2018


Mashabiki wa timu ya Simba wameshangazwa na kitendo cha uongozi wa Azam FC kuruhusu wapinzani wao kutumia basi lao, Mbabane Swallows FC watacheza leo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbabane Swallows jana walifanya mazoezi katika uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuweza kuikabili Simba walitumia basi la Azam FC ambalo liliwapeleka na kuwarudisha.


Uongozi wa Azam FC haujazungumzia jambo hilo ambalo huwa ni nadra sana kuweza kufanyika kwa nchi nyingine hasa timu zetu zinapokwenda kucheza huko.



Hata hivyo taarifa zinaeleza kwamba Mbabane walikodi basi hilo kwa uongozi wa Azam FC kwa ajili ya matumizi yao wanapokuwa hapa nchini kujiandaa na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mashabiki waliozungumza na SALEHJEMBE, walisema wanaingiwa hofu kuona wageni wakiwa katika basi hilo la Azam FC, jambo ambalo wanaona inaweza kuwa rahisi Waswazi hao kupata nafasi ya kujua mambo kadhaa ya Simba.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic