November 28, 2018


 Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa yupo tayari kupambana na JKT Tanzania kesho katika mchezo wa ligi kuu ila atawakosa wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza.

"Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Juma Mahadhi, Baruan Akilimali pamoja na Beno Kakolanya hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachocheza dhidi ya JKT Tanzania kwa kuwa wapo ambao ni majeruhi pamoja na sababu nyingine.

"Papy Tshishimbi tayari ameanza mazoezi ila hatakuwa na nafasi ya kuanza kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia kubwa,mchezo utakuwa mgumu ila tunahitaji pointi tatu," alisema.

Yanga wamekuwa na mwendelezo mzuri kwenye michezo waliyocheza ligi kuu mpaka sasa kwani katika michezo 12 waliyocheza wametoa sare 2 na kushinda michezo 10, wamefikisha pointi 32.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic