November 6, 2018


Inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amepanga kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Marcel Kaheza.

Aussems ameamua kufanya maamuzi hayo ili kumpa nafasi zaidi ya kujiweka vizuri Kaheza ambaye amekosa nafasi kutokana na upana wa kikosi cha Simba.

Taarifa za ndani zinaeleza Aussems amekuja na mbinu hiyo ya kumsaidia Kaheza japo kwa sharti la kucheza kikosi cha kwanza kule atakapoelekea.

Mchezaji huyo amekuwa hapati namba ndani ya kikosi cha kwanza tangu asajiliwe akitokea Majimaji FC na badala yake amekuwa akiingizwa katika baadhi ya mechi kipindi cha pili.

1 COMMENTS:

  1. Ni fursa nyingine kwa Marcel kama atatumia vizur nafac hyo, aongeze physique, left footer ni adimu sana!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic