MCHEZAJI UNITED ALALAMIKIA KUPIGWA CHINI NA MOURINHO
Nahodha wa Manchester United Antonio Valencia, 33, anadai kuwa meneja wake Jose Mourinho amemtema kama nahodha wake na kwamba hana jeraha lololote. (Area Deportiva, via Mail)
Winga wa Real Madrid Mcolombia James Rodriguez huenda akajiunga na ligi ya Primia msimu ujao wa joto.
Barcelona imesisitiza kuwa haina mpango wa kumuuza winga wake Ousmane Dembele, na kwamba haijapata ofa yoyote kumhusu. (Cadena Ser, via Evening Standard)
Chelsea inajiandaa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Christian Pulisic,20,- Wanapania kukamilisha usajili huo kufikia Januari. (Mail)
Beki wa Napoli Elseid Hysaj, 24, huenda pia analengwa na Chelsea, kwa mujibu wa ajenti wake. (Radio CRC, via Sun)
Juventus imeungana na AC Milan kuonyesha azma ya kumnunua kiungo wa kati wa Liverpool Fabinho 25. (Sport Mediaset, via Talksport)
Galatasaray inataka kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi kwa mkopo mwezi Januari. (ESPN)
Wolves anataka kumpatia Origi mkataba wa kudumu, na tayari wameweka dau la euro milioni 20. (Mirror)
Mlinzi wa Arsenal Julio Pleguezuelo, 21, amesema kuwa amepokea ofa kadhaa za kurejea Uhispania lakini anataka kuendelea kusalia Emirates. (Marca - in Spanish)
Tottenham wameonywa kuwa uwanja wao mpya huenda usiwe tayari kutumika hadi mwezi Machi kutokana na changamoto za hapa na pale katika eneo la ujenzi. (Times)
Kiungo wa kati wa Liverpool na England Alex Oxlade-Chamberlain, 25, anapania kurujea uwanjani baada ya kuumia goti mwishi wa msimu uliyopita. (BetVictor, via Liverpool Echo)
Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani ameahidi kuwapeleka wachezaji wake Las Vegas ikiwa watafaulu kupanda daraja na kujiunga na ligi ya Primia.(Mail)
Meneja mpya wa Fulham Claudio Ranieri amewafurahisha wakubwa wake wakati wa mahojiano ya kazi baada ya kuwaelezea kinaga ubaga kwa nini timu hiyo haifanyi vizuri na ni wapi panastahili kufanyiwa ukarabati. (Mail)
Teknolojia ya VAR au ya kutumia video kutoa uamuzi itaanza kutumika katika ligi kuu ya England msimu ujao baada ya vilabu vinavoshiriki ligi hiyo kukubaliana kimsingi.
Tayari majaribio yamekuwa yakifanywa katika baadhi ya mechi za msimu huu.
Wasimamizi wa mechi za ligi hiyo wanatarajiwa kutuma ombi rasmi kwa bodi ya kimataifa ya kandanda na shirikisho la kandanda duniani FIFA.
Klabu ya Chelsea huenda ikafungiwa kufanya usajili kwa miaka miwili ikiwa itapatikana na hatia ya kukiuka kanuni za usajili.
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment