MKWASA ASHINDWA KUVUMILIA, AWAIBUKA TFF
Baada ya juzi Jumamosi Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza majina ya waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa Yanga, huku ikisisitiza kutomtambua Yusuf Manji kama mwenyekiti wa klabu hiyo, aliyekuwa katibu mkuu wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa ameibuka na kutoa neno.
Mkwasa ambaye hivi karibuni aliachana na nafasi yake ya ukatibu mkuu wa Yanga ili akatibiwe tatizo la moyo lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu, ameliambia Championi Jumatatu kuwa TFF isiuchukulie poa mgogoro uliopo sasa kati yake na Yanga kuhusiana na Manji.
Mkwasa alisema licha ya kuwepo kwa upungufu mbalimbali wa kikatiba juu ya suala hilo, TFF inapaswa kutumia busara ili kuhakikisha Yanga inakuwa sawa na siyo kusababisha mvurugano.
“Kama Manji amekubali kurudi katika nafasi yake ya uongozi kutokana na uamuzi wa wanachama wa Yanga walioutoa kwenye mkutano mkuu wa klabu uliofanyika mwezi Juni, mwaka huu, TFF inapaswa kukubaliana na maamuzi hayo kwani hata katiba ya klabu inasema kuwa wenye maamuzi ya mwisho juu ya jambo lolote lile ni wanachama kupitia mkutano mkuu.
“Nakumbuka katika mkutano huo, mimi ndiye nilikuwa katibu ambapo wanachama kwa pamoja waliikataa barua ya kujiuzulu ya Manji na wakanitaka niwaandike barua ya kutaarifu kuhusiana na uamuzi wao huo, nilifanya hivyo na barua nyingine nikaipeleka TFF na katika mamlaka nyingine.
“Baada ya TFF kuipokea barua hiyo ilibidi wamwondoe aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa klabu yaliyofanywa na wanachama ya kugomea barua ya kujiuzulu kwa Manji, kwa hiyo hana sifa za kuwa katika nafasi hiyo kwa sababu Manji bado ni mwenyekiti Yanga.
“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo, TFF inapaswa kutumia busara kulimaliza tatizo hilo kwa faida ya soka la Tanzania hata kama kuna upungufu wa kikatiba ambao haukufuatwa ambao wao ndio wanasimamia lakini mwisho wa siku wenye maamuzi na Yanga ni Yanga wenyewe, tena kupitia mkutano wao mkuu,” alisema Mkwasa ambaye kwa sasa hafanyi kazi yoyote kutokana na ushauri aliopewa na madaktari wake waliokuwa wakimtibu tatizo la moyo lililokuwa likimsumbua.
CHANZO: CHAMPIONI
Mkwasa tulia uuguze moyo wako, usitafute balaa, Manji sio bubu ila tunamgeuza Mungu
ReplyDeleteMi naungana na wanachama, wapenzi na washabiki wanaotaka uchaguzi ufanyike. Timu imeendeshwa kiholela kwa muda mrefu sasa. Sidhani kama kuna mantiki ya kutofanya uchaguzi. Kama Manji anataka kuendelea anatakiwa atoke na kutoa kauli yake mbele ya wanachama na washabiki wote na hata Taasisi inayosimamia michezo nchini. Wachezaji wamekosa morali kwa kuwa hawajui kuhusu kesho. Endapo kama mishahara na mazingira mengine ya kazi yangekuwa yanaendelea vizuri tungesema ngoja tuvumilie.
ReplyDeleteTufanye uchaguzi na tuache propaganda za mpira zipite. Wasiotaka maendeleo bado wataendelea kumkumbatia Manji kama mwenyekiti. Upande wangu naona kabisa kama Manji anataka kurudi arudi kuwa mwekezaji na si mwenyekiti tena
1. Kabla ya uchaguzi huo mmejiandaaje ukigeuka kuwa uchafuzi badala ya uchaguzi?
Delete2. Wakati huu wa kipindi cha mpito na dirisha la usajili likiwa wazi mnaisaidiaje klabu yenu?
3. Je TFF ilipomuondoa Sanga ilimaanisha nini? Mamlaka nyingine kwanini zilikaa kimya wakati wote huo? Je ni maslahi ya nani Yanga kukiwa na mgogoro?