November 27, 2018


Simba ipo ka­tika maandalizi makali ya mechi yake ya Juma­tano ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swal­lows kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kocha Mbel­giji, Patrick Aussems amewapa kazi maalumu viungo wake wawili, Jo­nas Mkude na Mzambia, Cletus Chama.

Mkude alisema kuwa Aussems amefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya Mbabane Swallows.Alisema katika uchunguzi huo alibaini kuwa Mbabane wapo vizuri sehemu ya kiungo, ndiyo maana akaamua kuwapatia kazi maalumu.

“Kwa sasa tunaendelea kujifua vilivyo ili tuweze kuwa fiti tayari kwa kuifanya kazi hiyo am­bayo kocha ametupatia, ni matumaini yangu kuwa ha­tutamwan­gusha kocha, tutaifan­ya kama anavyotaka.

“ Kazi yenyewe hiyo kwa sasa si­wezi kuisema ila kwa yeyote atakayekuja uwanjani siku hiyo ataiona,” alisema Mkude ambaye hucheza nafasi ya kiungo mkabaji akishirikiana vilivyo na Mghana, James Kotei.

Kwa upande wake Cha­ma yeye hucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji anaye­tokea pembeni sawa na Shiza Kichuya.

Wakati huohuo, Mbabane wanatarajiwa kutua nchini leo Jumanne saa 7 usiku kwa ajili ya mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic