November 28, 2018

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Jaffary Kibaya ambae jana aliweka rekodi ya kufunga 'Hat-trick' kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Northen Dynamo ya Shelisheli ameahidi makubwa kwa mashabiki.

Mtibwa walishinda mchezo wao wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 matokeo yanayowapa nafasi kusonga mbele endapo hawataruhusu bao mchezo wa marudiano.


"Namshukuru Mungu kuweza kutusaidia kuibuka na ushindi na kufanikiwa kuifikia rekodi ya Joseph Kaniki hivyo nitaongeza juhudi zaidi katika michezo mingine kupata ushindi kwa ajili ya taifa, mashabiki watupe sapoti," alisema.


Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Desemba 5 ambapo ili Mtibwa waweze kuvuka hatua hii wanatakiwa wasiruhusu kufungwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic