Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Niyonzima amekiri kwamba kiungo mwenzake Claytous Chama anaujua mpira vizuri, ila anamzidi uwanjani kutokana na kutofautiana vitu vidogo ambavyo Chama hana.
Chama tangu amejiunga na Simba akitokea Power Dynamos ya Zambia amekuwa akifananishwa kiuchezaji na Niyonzima ambaye msimu huu hajawa na nafasi ndani ya Simba.
"Mimi na Chama ni marafiki na tunazungumza vizuri tofauti na wengi wanavyofikiria hasa kuhusu masuala ya uwanjani, Chama ni kiungo mzuri anajua mpira ila hatufanani.
"Yeye vile vitu anavyofanya uwanjani anafanya kwa uzito fulani hivi tofauti kabisa na mimi ambaye ninavifanya hivyo kwa uharaka hivyo hatuwezi kuwa sawa hata kidogo," alisema.
Niyonzima amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba, hajaweza kufanya vizuri tangu asajiliwe Simba msimu uliopita akitokea Yanga.
Kutoka Championi
Mbona humuonesh kocha akakupanga japo dk 1 kula siku porojo tu
ReplyDelete