November 28, 2018

Mshambuliaji  wa timu ya Azam FC, Ramadhani Singano 'Messi' ambaye alikuwa ni mfungaji wa bao la ushindi kwenye mchezo wa Azam FC dhidi ya Mbabane Swallows FC waliocheza mwaka 2017 wa ligi ya Mabingwa wa Afrika amewapa mbinu washambuliaji wa Simba kuiua Mbabane leo.

Simba wanacheza na Mbabane ya Swaziland uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kimataifa na mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 4 au 5 safu ya washambuliaji inaongozwa na Meddie Kagere, Emanuel Okwi na John Bocco.


 Singano alisema kuwa Simba wanapaswa wawe na nidhamu ya juu watakapokutana na Mbabane hasa kutokana na mbinu zao ambazo hazitabiriki uwanjani.

"Wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu wakiwa uwanjani na wanapaswa watumie vizuri wenyeji wao kwa kuwa ni fursa kwao kuweza kupata matokeo mazuri hapa na nina amini wanaweza kufanikiwa.


"Washambuliaji wao wanapaswa kutulia hasa wanapofika kwenye lango la mpinzani, hakuna timu isiyofungika naamini wakiwa makini kutumia nafasi watakazotengeneza itawafanya wapate matokeo na inawezekana," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic