November 28, 2018

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kusajili kutokana na wachezaji wengi waliopo ndani ya Yanga kudai fedha za usajili.

Zahera amewaambia viongozi kwamba huwezi kuongeza wachezaji wapya kwenye timu ilihali wale ambao wapo ndani ya timu hawajakamilishiwa stahiki zao.


"Siwezi kusajili wachezaji wapya ndani ya timu kwa sasa wakati kuna wachezaji wasiopungua kumi wanadai fedha zao za usajli, nimewaambia viongozi kama watashindwa kumaliza matatizo ya wachezaji waliopo hatutasajili wachezaji wapya mpaka matatizo ya wachezaji waliopo yaishe," alisema.


Miongoni mwa wachezaji ambao wanadai uongozi imeelezwa kuwa ni pamoja na golikipa Beno Kakolanya na Kelvin Yondani ambao walishindwa Kujiunga na timu kwenye michezo ya kanda ya Ziwa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic