November 7, 2018


Na George Mganga

Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi na Mwanachama wa Yanga, Ridhiwani Kikwete amesema ameshangazwa na walichokifanya wanachama Yanga kwa kupinga kusimamiwa uchaguzi na Kamati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

AKizungumza na Radio EFM asubuhi hii, Ridhiwani ameeleza kuwa ifikie hatua wanayanga wakubali kubadilika na kutengeneza maendeleo kwa faida ya klabu.

Mwanachama huyo amesema Yanga imekuwa ikiendeleza malumbano ambayo hayana msingi na mpaka TFF imefikia hatua ya kuingia mchakato wa uchaguzi wa klabu yao.

Ameongeza kwa kuwataja watani zao wa jadi Simba kuwa juzi tu wamekamilisha kufanya uchaguzi wao vema na akiwaomba wanayanga ni vizuri wakaiga jambo hilo kwa maslahi mapana ya klabu.

Kauli ya Ridhiwani imekuja kufuatia mkutano wa matawi Yanga uliofanyika jana kupinga vikali suala la klabu kusimamiwa uchaguzi na TFF ambalo amelichukulia kama si jambo zuri kwa namna walivyozungumza.

2 COMMENTS:

  1. KWAHIYO KUIGA NDIO KUSIMAMIWA NA TFF KWENYE UCHAGUZI/MBONA SIMBA WAMEFANYA UCHAGUZI KWA KAMATI WALIYOITEUA WENYEWE?ACHENI KUHIDHOOFISHA YANGA KUPITITIA TFF KWANI WOTE TUNAFAHAMU KUWA HAO BMT,TFF NI SIMBA WA ASILI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndugu, BMT walishatoa reason kuwa Yanga Uongozi haujakamilika thats y Tff kama mlezi watasimamia, haina Mwenyekiti,Makamu na wajumbe 4 wanamiss hivyo hawajitoshelezi kusimamia uchagizi, hata Katibu Kaaya ana kaimu!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic