November 7, 2018


Tawi la Yanga la Manzese la jijini Dar es Salaam limeibuka na kutoa tamko lao kuwa, wao wanafahamu Yusuf Manji bado ni mwenyekiti wao huku likilitaka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lisiwaingilie kwenye uchaguzi.

Kauli hiyo, wameitoa ikiwa ni siku moja tangu TFF itangaze tarehe ya uchaguzi ya Yanga ambayo ni Januari 13, 2019 kwa ajili ya kujaza baadhi za nafasi za wajumbe na mwenyekiti.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, katibu mkuu wa tawi hilo, Shabani Omary, alisema wao wanashangaa kuona BMT na TFF wakiwaingilia masuala mbalimbali likiwemo la kutamka hawamtambui Manji.

Omary alisema, Manji bado anafanya kazi za klabu kama kawaida na hilo limethibitishwa na viongozi wao, hivyo hawataki kuingiliwa katika hilo huku wakiwaomba wanachama wa klabu hiyo kutojitokeza TFF kwenda kuchukua fomu za kugombea.

“Ujue tunashindwa kuelewa, kama unakumbuka hivi karibuni TFF ilisema kuwa inamtambua Manji ndiyo mwenyekiti wetu na ndiyo sababu ya kumuondoa aliyekuwa ana kaimu nafasi ya Manji baada ya kuandika barua ya kujiuzulu katika nafasi hiyo kabla ya Sanga (Clement) kuondolewa.

“Kingine katika mkutano mkuu wa Yanga uliohudhuriwa na Waziri Mwakyembe (Harrison), wote kwa pamoja wanachama tuligomea barua ya Manji aliyoiandika kwa viongozi wa Yanga tukitaka kuendelea na Manji, hivyo tunashangaa kuwaona BMT na TFF wakiingilia mambo yetu wakisema hawamuoni akifanya kazi.

“Sasa hao BMT na TFF wanataka kumuona Manji akifanya kazi huko kwao? Sisi tunajua Manji anafanya kazi na Yanga na mara kadhaa amekuwa akikutana na viongozi akina Kaya (Omary) ambaye ni kaimu katibu, tunawaomba watuachie Yanga na Manji wetu, basi kama ni uchaguzi, uitishwe mkutano wa dharura kwanza,” alisema Omary.

7 COMMENTS:

  1. Manji Manji hakuna jambo lingine la kuibadilisha Yanga zaidi ya kumtegemea Manji. Mlishindwa kumtetea wakati anataka kuikodisha Yanga mkaa kimyaa

    ReplyDelete
  2. Wanachama na Mashabiki wa acheni ujinga na mtambue kuwa Yanga ni klabu ya wananchi na ililuwepo kabla hata Manji Kuzaliwa na ilifanya vizuri kuliko sasa. Wanachama Yanga hasa mnayelazimisha aendelee Manji kuwa Mwenyekiti ni Mambumbu kwasababu yeye ametumia haki yake ya Kikatiba kwa kuandika barua ya kujitoa kwenye Uongozi kutoka na majukumu kumbana na kwa maslahi Mapana ya Klabu apatikane mwingine atakyeipeleka Yanga Mbele. Igeni wenzenu Simba wala msione aibu kwasababu kaaza mtani wenu na ni lazimu muwe na wivu wa kimaendeleo sio wa kutafuta mchawi wa kuloga ili fulani asifanikiwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWANI TFF NA BMT WAMEICHANGIA YANGA SH.NGAPII KWENYE BAKULI LAO ? MAANA YANGA WANATEMBEZA BAKULI.NA HUENDA NI VEMA WANGEWEKA WAZI MICHANGO YAO KWA YANGA KABLA YA KUWAINGILIA YANGA NA MAMBO YAO.

      Delete
    2. Angalia husije wewe kuwa mjinga wa kwanza

      Delete
    3. mchango wa Tff kwa Yanga ni kuipangia mechi nyingi @home ground Taifa

      Delete
    4. Duh...hii kali

      Delete
    5. Kwa maana ya kukusanya mapato ya mlangoni kwa mwenyeji kuchukua mapato yote?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic