November 7, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Ndada FC, Malale Hamsini amesema kuwa KMC waliwaokota ndio maana wakafanikiwa kuchukua pointi tatu, kwa sasa hakuna timu itakayofanikiwa kushinda mbele yake atadhihirisha hilo leo mbele ya Coastal Union.

Ndanda walifanikiwa kutoa sare na Yanga ambayo ipo kwenye ubora kwa sasa hali iliyofanya Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kuwalaumu washambuliaji wake kwa kukosa umakini.

Hamsini amesema kuwa mpira ni mbinu hasa katika kutafuta matokeo, wachezaji wake wanazidi kuimarika hana hofu na timu zinashoriki ligi Kuu kwa sasa.

"Mwanzo nilianza kwa kusuasua kwa kuwa wachezaji walikuwa bado hawajazoena ila kwa sasa mbinu zimeshajibu ni muda wa kusubiri matokeo kila tunaposhuka uwanjani tumejipanga kuchukua pointi tatu," alisema.

Ndanda imefanikiwa kugawana pointi moja na timu zote vigogo kwa kuanza kutoa sare ya kutofungana na Simba kisha wakafuata Yanga kwa kutoa sare ya kufungana bao 1, leo itacheza na Coastal Union uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic