Imeelezwa kuwa sababu kubwa za Kocha Mkuu wa Simba ,Patrick Aussems kutaka kusajili mbadala wa Jonas Mkude ndani ya kikosi chake ni kutokana na uhalisia alionao Mkude tofauti na James Kotei ambaye sio kiungo mkabaji halisia.
Aussems alitoa mapendekezo kwa uongozi wake akihitaji kufanyiwa usajili wa wachezaji wawili ambao ni beki pamoja na kiungo mkabaji ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chake.
"Kocha anataka kuongeza nguvu ndani ya kikosi kwa kuwa alipata tabu Mkude alipoumia huku Kotei alikuwa na adhabu aliyopewa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) hivyo kumlazimu kumtumia Said Ndemla ambaye si kiungo mkabaji halisi," kilieleza.
Aussems alisema kuwa ana mpango wa kufanya usajili kwa katika dirisha dogo ila hawezi kutaja ni nafasi gani kwa sasa kama itakuwa ni kuingo mkabaji ama beki itajulikana.
"Siwezi kusema kwa sasa ni nafasi gani kama ni hiyo ya kiungo mkabaji basi itajulikana nitakapokuwa nimekamilisha zoezi hilo," alisema.








Mlipili angeitumia fursa hiyo. Awe kiungo mkabaji apate namba
ReplyDelete