Uongozi wa timu ya Singida United umesema kuwa upo kwenye mazungumzo na wachezaji wanne wa kimataifa ili kuweza kuongeza nguvu katika kikosi chao kwenye dirisha dogo la usajili ili kuongeza nguvu.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amesema kuwa watatumia dirisha dogo kufanya maboresho makubwa ya kikosi ili kuweza kuleta ushindani katika ligi kuu pamoja na shindano la SportPesa Cup ambalo litafanyika Januari mwakani.
"Tupo kwenye mazungumzo na wachezaji wanne wa kimataifa ambao tutawaongeza ndani ya timu yetu kwa sasa, pia kuna wachezaji ambao wanaweza kuondoka dirisha dogo, nasi tumejipanga kuleta wachezaji ambao watakuwa mbadala wao.
"Tayari tumewaandikia Simba kuomba mchezaji wao mmoja ili aweze kujiunga katika timu yetu kwa ajili ya kuongeza nguvu, tunaamini tutafanya vizuri ," alisema.
Baadhi ya wachezaji waliotimka kikosini hapo ni Miraj Adam, Jamal Mwambeleko, Manyika Pete, Shafiq Batambuze, Michael Rusheshangoga, Danny Usengimana na Tafadzwa Kutinyu.








0 COMMENTS:
Post a Comment