November 28, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umemtambulisha mchezaji mpya, Zana Coulibaly, kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Simba wametangaza kuwa beki huyo ndiye atakuwa mbadala wa Shomari Kapombe ambaye ameumia hivi karibuni akiwa na kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' wakati kikijiandaa na mechi ya kufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Lesotho.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Simba wameandika kuwa mchezaji huyo atawasili nchini kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho ili kujiunga na timu yao.

Tunapenda kuwatangazia kwamba beki Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast leo atawasili nchini kwa ajili kukamilisha taratibu za mwisho kujiunga na timu yetu ili kuziba pengo la beki Shomari Kapombe ambaye siku za karibuni alipata majeraha

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic