November 13, 2018



Michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajia kuanza kutimua vumbi Januari 2019, imeisogeza karibu mechi ya Simba na Yanga kufuatia kupangwa pamoja katika michuano hiyo inayozishirikisha timu kutoka  Kenya na Tanzania ambapo mshindi wa michuano hiyo atavaana na Everton ya England.

Michuano ya SportPesa inatarajia kuzinduliwa kwa mara ya tatu ambayo awali ilianza rasmi mwaka  2017 ambapo timu ya Gor Mahia kutoka Kenya ndiyo iliibuka na  ushindi kwa mara zote mbili hivyo kuvaana na Everton.

Timu zinazotarajia kushiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Simba, Yanga, Singida United na Mbao FC kwa upande wa Tanzania wakati kwa upande wa  Kenya timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, Kariobangi Sharks, Bandari FC na AFC Leopards.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa , Tarimba Abbas amesema kuwa timu nane kutoka Kenya na Tanzania zitashiriki katika michuano hiyo itakayotumia wiki moja huku bingwa akipatiwa kitita cha dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 60) pamoja na kucheza na Everton.

“Awamu ya tatu ya michuano ya SportPesa Super Cup inatarajia kuchezwa jijini Dar, Januari mwakani kwa kushirikisha timu nane kutoka Kenya na Tanzania  ambayo itachezwa ndani ya wiki moja, hii itakuwa ni awamu ya tatu tangu ilipozinduliwa mwaka 2017 ambapo Gor Mahia ndiyo imeibuka mshindi kwa mara zote hizo.

“Michuano hii imekua na mafanikio makubwa na imeweza kusaidia kuinua kiwango cha klabu pamoja na wachezaji wetu. 

“Mshindi wa michuano ya Super Cup atajizolea kitita cha Dola 30,000 pia atacheza na Everton kutoka Uingereza, mshindi wa pili atachukua dola 10,000 na wa tatu atachukua Dola 7,500 wakati wa nne atajinyakulia kitita cha Dola 5,000 na timu zitakazofanikiwa kufika hatua ya robo fainali zitapata Dola 2,500 kila moja,” alisema Tarimba.


Aidha, kwa upande wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao alisema kuwa  michuano hiyo ni chachu ya kuwajengea wachezaji hali ya kujiamini na uzoefu wa mechi za kimataifa huku kwa upande wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaya amesema kuwa michuano hiyo ni kipimo tosha kwa wachezaji wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic