Dozi ya kikosi cha Taifa nchini Afrika Kusini, kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Lesotho, ikiwa ni maandalizi ya kuitafuta tiketi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Ligi ya Mataifa ya Afrika (Afcon) ni ya nguvu kwa kuwa wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku.
Meneja wa Taifa Stars, Dany Msangi amesema kuwa wachezaji wote wana ari ya kupambana kwa kuwa wanatambua wametumwa kazi na taifa linawategemea.
"Wanaendelea vizuri kuelekea Afcon hivyo wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku ili kuwa na pumzi ya kutosha pamoja na kupata mbinu nyingi za mwalimu, mashabiki waendelee kutupa sapoti na kutuombea," alisema.
Stars ipo kundi L mchezo wao utachezwa Novemba 18, 2018 Maseru, Lesotho ukiwa ni wa marudiano na fainali ya mashindano hayo yatafanyika nchini Cameroon mwakani .
0 COMMENTS:
Post a Comment