SIMBA YAPANGIWA KUCHEZA NA WABABE WA SWAZILAND LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Na George Mganga
Klabu ya Simba imepangiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Mbambane Swallows ya Swaziland.
Mechi ya kwanza itafannyika jijini Dar es Salaam kati ya terehe 27-28 Novemba 2018 na ya marudiano itapigwa huko Swaziland 4-5 Disemba 2018.
Mechi hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa Simba msimu huu na pia itakuwa inaanza kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada ya kuikosa kwa takribani miaka mitano nyuma.
Wakati huo kikosi cha Simba kimeendelea kujifua na mazoezi jijini Dar kwa ajili ya mechi zake zijazo za ligi ikiwa sambamba na maandalizi ya kuelekea mashindano hayo ya kimataifa.
Kila la kheri Simba SC...wababe wa Tanzania, washindani katika Ligi ya Mabingwa Afrika....wawakilishi kutoka Tanzania....wazee wa tano tano....wakali wa Kariakoo. Tunakwenda kupiga sasa ule mpira wa Kibabe...tunawaoneshe safari hii kuwa nasi tunaweza angalau Timu kama Mbabane Swallows si timu ya kuibeza sana. Mbabane Swallows ndipo alipotokea Asante Kwasi na Mwenzio Tshishimbi...wana wachezaji wanaojua mpira kuliko tunavyoweza kuitaja Club yao. Tunatakiwa tusiwabeze ila tunatakiwa tuwaoneshe kuwa sisi ni wakali wa Tanzania.
ReplyDeleteMbabane Swallows..najua wengi wanajua kuwa ndio Timu iliyoitoa Azam kwenye Kombe la Shirikisho baada ya hapa kufungwa na Azam alafu wakaenda kupindua matokeo kwao kwa kuwafunga Azam. Ni timu yenye ushindani na wanajua angalau sisi tunajua zaidi.
Tuwachukulie kuwa wao ni Mabingwa ila sisi ni mabingwa zaidi yao...tunaweza. Ni timu ambayo ipo kwenda ukanda wa timu za Afrika ya Kusini kwa hiyo wana kiutamaduni wa aina ya mfumo wa mpira unaoitwa "Shibobo"..ni aina ya mpira wa burudani na magoli.
Kila la Kheri Simba
Watanzania wote hasa wapenda Soka na si washabiki maandazi tunawaunga mkopno kwa kuwa kufanikiwa kwenu kutaleta ongezeko wa timu kutoka Tanzania kwenye mashindano makubwa. Niwape nguvu kwa maana na kwa imani mnaweza kwa kuwa mna kikosi chenye ushindani. Tushindane na tupiganie Tanzania yetu na kuondokana na kuchekwa na nchi zingine.
Kwahyo timu itakayo fungwa apo ndio bas au
ReplyDeleteKwahyo timu itakayo fungwa apo ndio bas au
ReplyDeleteTimu itakayofungwa inaaga mashindano. Hii ni hatua ya mtoano siyo makundi
ReplyDelete