November 9, 2018


Mkali wa asisti ndani ya Ligi Kuu Bara, Ibrahim Ajibu ambaye mpaka sasa amefikisha tisa akiwa na mabao matatu amesema kuwa kwake moto hauzimi kutokana na maneno ambayo anaambiwa na kocha Mkuu Mwinyi Zahera kumpa hasira zaidi.

Zahera amekuwa akimwambia Ajibu kuwa bado haonyeshi juhudi akiwa uwanjani licha ya kuwa msaada akiwa ndani ya uwanja jambo ambalo limekuwa likipokelewa kwa utofauti na Ajibu.

“Maneno yake huwa yananiumiza moyo lakini yananipa hasira na nguvu ya kupambana hasa nikiwa uwanjani hata nje ya uwanja bado najifunza muda wote ili kuwa bora zaidi ya jana nikiwa ndani ya uwanja.

“Ushindani ni mkubwa kwa sasa nasi tunajitahidi kufanya vizuri na yote yanawezekana kwa kuwa tumeshatengeneza muunganiko mzuri ambao unatusaidia tupate matokeo mazuri na hilo ni jambo la faraja kwetu, mashabiki watupe sapoti,” alisema Ajibu ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.

Viungo washambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngassa jana asubuhi wameripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo huku wakikanusha taarifa za kugomea mazoezi.

Katika mazoezi ya juzi wachezaji wanne wa timu hiyo Ajibu, Andrew Vicent ‘Dante’, Matheo Antony na Mrisho Ngassa hawakuonekana katika mazoezi huku taarifa zikienea wameweka mgomo kwa kile kilichodaiwa ni madai ya mishahara yao ya miezi minne wanayodai. Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema wachezaji hao walikuwa na matatizo tofauti.

9 COMMENTS:

  1. Mishahara tena mbona Yanga mnatia aibu !?

    ReplyDelete
  2. Na bado mbona wataumbuka mwaka huu.

    ReplyDelete
  3. Na bado mbona wataumbuka mwaka huu.

    ReplyDelete
  4. Na ndiyo wanaondoka Dar hivyo!

    ReplyDelete
  5. Mbona kila wachezaji wa Yangu wakikosa mazoezi kwaajili ya matatizo binafsi huyo Ajibu lazima awepo?

    ReplyDelete
  6. Kwa nn msijadili mambo ya timu zenu na mnaijadili Yanga? Timu zenu kwan zipo vzr?

    ReplyDelete
  7. Kwa nn msijadili mambo ya timu zenu na mnaijadili Yanga? Timu zenu kwan zipo vzr?

    ReplyDelete
  8. Kwenye ile kampeni ya kuchangia timu ya wananchi mimi nilitoa buku , na pia baada ya kufunzu katika magrupu caf tulipewa milioni 600 , nataka kesho wachezaji walipwe mishahara yao , vinginevyo viongozi nitawafungulia kesi ya utakatishaji fedha

    ReplyDelete
  9. Hongera Ajibu.Angalau Sasa namwona Ajibu Mpya,abayependa kusoma toka Kwa mwalinu wake ili kumletea ubora na matokeo mazhri ktk gani yake.Bafikiri mashabiki na Mgazeti has in ups banks he na mwalimu wako.Ukitulia na kuvumilia unaweza kuokota kitu cha kukusaidia ktk maisha yako ya kisoka.usikuzwe kichwa na mgazet Bali msikilize mwalimu wako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic