Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kikosi chao kimezidi kujifua zaidi kuelekea mechi yao na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Simba itakuwa na kibarua hicho chenye ushindani wa aina yake kati ya Novemba 27-28 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo itawakaribisha miamba hao.
Kuelekea mechi hiyo Manara ameeleza kuwa Mbabane wako vizuri hivyo ili kufanya vema ni vizuri wakajipanga vilivyo na hawatoichukulia utani mechi hiyo.
Tayari kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi kimezidi kujifua kuelelea mechi hiyo huku Kocha wake Mbelgiji, Patrick Aussems, akiwapa tizi la maana vijana wake.
Baada ya kukipiga hapa nchini tarehe tajwa hapo juu, Simba watasafiri kuelekea Swaziland ambapo watacheza mechi ya marudiano kati ya 4-5 Disemba mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment