November 15, 2018


Siku ya Ijumaa Novemba 16, 2018 nyasi za uwanja wa Taifa zitapata tabu kufuatia timu ya soka Tanzania bara ambayo pia ni mabigwa wa Ligi Kuu Bara, SimbaSC watamenyana na mabigwa wa ligi soka nchini zambia Big bullets. 

Mtanange huo unategemewa kushuhudiwa na wapenda soka wengi nchini kutokana na bei za majukwaa kuwa ya gharama nafuu zaidi.

Akitangaza bei ya kushuhudia mtanange huo, Msemaji mkuu wa Simba, Haji Manara amesema kuwa bei za viingilio ni shilingi elfu tatu (3000), elfu saba (7000) na elfu kumi (10000).

Kuwatoa hofu mashabiki wa simba manara amesema " kwa sasa tuna kikosi kikubwa ambacho licha ya baadhi ya wachezaji kwenda timu ya taifa tutafanya vizuri".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic