Uongozi wa Singida United, umesema kuwa bado haujakamilisha utaratibu wa kumtambulisha mshambuliaji mpya kutoka nchini Noryway na kuwataka mashabiki wasiwe na papara.
Ofisa habari wa Singida United, Cales Katemana amesema wanafanya usajili kwa umakini kuweza kusuka kikosi upya hivyo baada ya kukamilisha taratibu kila kitu kitakuwa wazi.
"Kwa sasa bado hatujaingia mkataba na mchezaji kutoka Norway ila mipango hiyo ipo, mashabiki watulie wasiwe na papara kwa kuwa haya mambo yanahitaji utulivu," alisema.
Singida United wapo kwenye mpango wa kusajili wachezaji wapya wa kimataifa kutokana na kuondokewa na wachezaji wao kwa madai ya kukosa namba pamoja na wengine kuuzwa huku jina la Dauda B mwenye uraia pacha wa Liberia na Norway akidaiwa tayari ameshatia saini.








Acheni ujinga, mmeshindwa kuwamantain waliokuwepo mnakimbilia kutuambia mnorway, mnahisi mtapata kiki kisa mnorway?
ReplyDelete