November 22, 2018




Mchezo wa Ligi Kuu leo kati ya Yanga na Mwadui FC ya mkoani Shinyanga uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage, umemalizika na Yanga wakichukua pointi tatu baada ya kushinda kwa bao 2-1.

Yanga walianza kuandika bao la kwanza kupitia mshambuliaji wao Heritier Makambo dakika ya 10 akimalizia pasi ya Paul Godfrey na kuimalizia kwa guu lake la kulia.


Mwadui walipata bao lao dakika ya 40 lililofungwa na Salum Aiyee baada ya golikipa wa Yanga Klaus Kindoki kuutema mpira aliokuwa ameudaka.


Mrisho Ngassa anaandika bao la 2 dakika ya 56 baada ya mabeki wa Mwadui kufanya uzembe nje ya 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic