November 4, 2018


Timu ya Alliance FC ya mkoani Mwanza imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United katika mchezo uliochezwa uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na dakika ya 90 na Martini Kiggi  na kuwafanya Aliiance wafanikiwe kuchukua pointi tatu muhimu.


Huu unakuwa ni ushindi wa pili kwa timu ya Alliance kwenye ligi kuu bara kuwafanya wapande kutoka nafasi ya 20 ambayo walikuwa kwenye msimamo na kufika nafasi ya 17 baada ya kucheza michezo 13 na kukusanya pointi 10.


Ofisa habari wa Alliance FC James Mwafulango amesema kuwa huo ni mwanzo tu kwa kuwa michezo bado inaendelea kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki ili waweze kufanya vizuri.


"Tumeanza taratibu kurejea kwenye ubora wetu, tutatumia vizuri uwanja wa nyumbani na hata tukitoka tutafanya vizuri nina imani baada ya kutoka hapa kuna timu itapigwa mabao 7," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic