November 4, 2018


Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kilichowasaidia kuweza kuwashinda wapinzani wake Ruvu Shooting kwenye mchezo wao ligi kuu ni juhudi za wachezaji katika kuhakikisha kwamba wanaweza kuwafunga.

Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa bado Ruvu Shooting walikuwa wanasumbuliwa na kivuli cha mabao 5-0 waliyofungwa na Simba hivyo walikuwa wamepaniki na kupoteza umakini hali iliyowapa wepesi katika kupata matokeo.


"Wachezaji wamecheza vizuri wamejituma na kufanya kazi yao ipasavyo, bado wapinzani wetu walikuwa wanasumbuliwa na kupoteza mchezo wao uliopita ilihali sisi tulikuwa tumeshinda, tumetengeneza nafasi na tumezitumia.


"Bado tuna kazi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri kwa kuwa baada ya kumaliza mchezo kinachofuata ni kazi nyingine kwa ajili ya kuendeleza ushindi zaidi, kikubwa ni kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu," alisema.


Ushindi huo unawafanya Mtibwa Sugar kupunguza idadi ya mechi za kufungwa kwa kuwa tangu msimu wa 2013/14 wamekutana mara tisa huku ruvu wakishinda mara nne na Mtibwa wakishinda leo mara mbili na kufanya sare ziwe tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic