Mwenyekiti wa kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania iliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa miguu (TFF) Boniphace Wambura amezishauri timu zote kuweza kufanya usajili kwa kuzingatia ripoti ya benchi la ufundi.
Dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa 15 mwezi huu na kufungwa 15 Desemba ambapo linatoa ruhusa kwa timu kuweza kuongeza wachezaji ambao wanawahitaji kuongezea nguvu.
Hatua hiyo imekuja kutokana na utaamduni wa baadhi ya timu kufanya usajili wa kiholela bila kuzingatia mahitaji ya benchi la ufundi.
Kitendo hicho kimeifanya TFF iweze kukumbushia juu ya suala hilo ambalo limekuwa sugu jambo ambalo linapelekea wachezaji wengi wapya wanaosajiliwa kukaa benchi.
"Ligi haisimami kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo kwa kuwa ni mpango maalumu kwa ajili ya kuweza kuwa kwenye ushindani, timu zinapaswa zifanye usajili kwa kuzingatia maelekezo ya benchi la ufundi ili kusaidia kuleta kile ambacho kinakosekana," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment