Mambo yanazidi kuwa magumu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na kukosekana kwa mdhamini mkuu timu nyingi zimekuwa zikisumbuliwa na tatizo la ukata na kushindwa kuwalipa stahiki zao wachezaji.
Stand United ni miongoni mwa timu ambayo haijakamilisha stahiki za wachezaji wengi wa timu hiyo hali iliyofanya wachezaji wengine kushindwa kuendelea wakisubiri kulipwa stahiki zao.
Habari kutoka ndani ya klabu zilieleza kuwa mambo bado hayajakaa sawa hasa kiuchumi hali ambayo inafanya wachezaji wawe katika mazingira hayo ila wanaamini muda utafika kila kitu kitakuwa sawa.
"Kwa sasa wachezaji wanadai stahiki zao hilo lipo wazi ila kama ambavyo unajua kwamba kuendesha klabu sio kitu chepesi, wakati utafika mambo yatakuwa sawa," alieleza.
Mmoja wa wachezaji wa Stand United, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia stahiki zao kwa muda mrefu lakini hakuna wanachopewa zaidi ya kuambiwa wasubiri.
"Mchezaji inabidi uwe na akili kichwani hasa kuweza kufikia malengo yako, bado sijakamilishiwa stahiki zangu na ninafurahia kuitumikia timu yangu nina amini siku moja malengo yangu yatatimia na nitaweza kucheza nje ya nchi endapo nitapata timu," alisema
0 COMMENTS:
Post a Comment