November 22, 2018

1 COMMENTS:

  1. Hao wanaomtetea kocha na kuwalaumu wachezeji labda ni wajomba zake na Karia raisi wa TFF wametunwa kuja kumtetea. Kocha anakuja na mbinu za kipumbavu za kumkabili adui timu inapigwa alafu watu wanakuja kuwaropokea wachezaji kama si uonevu kitu gani? Kweli watanzania tunatatizo la kujitoa kwa taifa letu lakini ifahamike pia hakuna mwanadamu atakaejitoa katika njia sahihi bila ya kupata muongozo sahihi wa kujituma kutoka kwa kiongozi anaemuongoza na ndio maana baada ya kujitambua yakuwa watanzania sio watu wa kujitoa hasa katika michezo au pengine hata shughuli nyengine ndipo nchi ikaingia gharama ya kumuajiri kocha wa kigeni tena kutoka Nigeria ili alete siri ya wachezeji kujituma na kujitoa wakiwa uwanjani maana wao wanaigeria wanafanya vizuri. Sasa tuwe wa kweli bila ya kuleta siasa kazi moja muhimu ya Amunike kama kocha ni hiyo ya kuwafundisha wachezaji jinsi ya kujituma kikamilifu aiza kwa timu yao au kwa taifa lao na kama kazi hiyo kashindwa kuifanya Amunike pale Taifa basi atafutwe kocha mwengine haraka. Waswahili wanamsemo unaosema usione vinaelea ukafikiri vinaelea bure bure tu,hapana huwa vimeundwa. Ukawaona Wachezaji wa Uganda wanajituma kwa Taifa lao ujuwe sio bure wamefundwa kutokana na kuwa na kocha bora walienae. Na ukitaka kuthibitisha ubora wa kocha wa Uganda basi nenda kachungulie wasifu wake wa kazi halafu linganisha na wasifu wa kazi wa kocha wa Taifa Stars. Ama kwa kutumia wasaa huu wa maoni yangu ningemuomba brother Saleh(Jembe) kama atakuwa hana nidhamu ya uoga atuanikie hadharani C.V za makocha wa Uganda, Kenya na Tanzania ili watanzania waelewe kiwango gani cha ufundi na uzoefu cha mwalimu wao wa timu yao ya Taifa kulinganisha na wenzetu hao niliowataja ya kenya na Uganda . Amunike hajaajiriwa kuja kufundisha Tanzania kuja kuuza jina lake kama baadhi ya watanzania wengi wanaozuzuka na jina lake bali ameajiriwa katika timu ya Taifa kuja kuleta ufundi na fundi ni fundi tu kwa maana yakwamba kukijenga kilichobomoka. Au kuunda kitu kipya kilichobora kuliko kilichokuwepo. Lakini kuna dalili zote yakuwa watanzania kwa Amunike tumepanda mkenge na Viongozi wasipochukua hatua mapema ya kurekebisha mapungufu basi kuna hatari Tanzania na Taifa stars tukavipoteza vizazi vya dhahabu vinavyonyanyukia hivi sasa. Ukichukulia vipaji vya hali ya juu kwa wachezaji vijana basi Tanzania ni kati ya nchi ambazo kuna vijana wengi sana wenye ari na njaa ya mafanikio ila tatizo ni kukosekana miongozo sahihi jinsi ya kuviendeleza vipaji hivyo. Na mbaya zaidi Tanzania hatujawahi kwa miaka ya hivi karibuni kumleta kocha ambae angalau ameshafika fainali ya klabu bingwa ya Africa seuze Afcon,kwa ajili ya timu ya Taifa. Tumekuwa tukioketezea makocha wa hovyo hovyo of course watatujengea misingi ya hovyo kwa wachezaji wetu halafu bila ya aibu tunawalaumu wachezaji kwa matokeo mabovu. Zahera wa Yanga yule pale licha ya ukata walionao Yanga na anafanya vizuri na wachezaji ni watanzania. Labda Amunike anawachukulia watanzania ni watu wasiokuwa na uelewa wa masuala ya soka ndio maana kaletwa yeye na anahaki ya kufanya vyovyote anavyoona sawa kwa sababu waliokuwepo hawajui lolote. Lakini siku Magufuli alipowaita taifa stars ikulu alisema neno moja ambalo siwezi kulisahau. Neno lenyewe ni hili, alisema kocha asiingiliwe au asichaguliwe wachezaji katika kupanga kikosi chake kwa sababu tukishindwa kupata matokeo tunayoyahitaji tutajua tatizo ni la kocha. Na ndipo leo nawaza na kufikiri how genius Magufuli was in that statement. Lakini la kushangaza leo timu ya Taifa imevurunda tunasema kocha sio tatizo? Ina maana kauli na maagizo ya muheshimiwa raisi hayakuwa na maana yeyote isipokuwa alipoteza muda wake for nothing na ikiwa hivyo ndivyo ilivyo basi watanzania tuna matatizo tena makubwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic