November 30, 2018


Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0jana  dhidi ya timu ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga waliandika bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Herieter Makambo dakika ya 20 akitumia vema makosa ya walinzi kisha bao la pili likafungwa na Mrisho Ngasa dakika ya 53 akimalizia pasi ya Rafael Daud na bao la tatu limefungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 79 kwa mkwaju wa penati.

Kwa matokeo haya Yanga wanawashusha Azam FC kwa kufikisha pointi 35 wakiwaacha kwa jumla ya pointi 2 Azam huku wakiwaacha kwa jumla ya pointi 8 wapinzani wao Simba wenye pointi 27.

Yanga wamecheza michezo 13 huku wakishinda michezo 11 na kutoa sare michezo 2 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic