November 6, 2018


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umeanza mchakato wa kuwania saini za wachezaji wawili kutoka Gor Mahia FC kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems anazihitaji.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza wachezaji Philemon Otien na Ephrem Guikan ndiyo wanaowaniwa kwa ajili ya usajili pindi dirisha dogo litakapofungulowa Novemba 15 2018.

Wachezaji hao wawili wanacheza nafasi tofauti ambapo Guikan anakipiga katika nafasi ya ushambuliaji huku Otien akicheza nafasi ya kiungo.

Usajili huo umekuwa pendekezo la Aussems ambaye amedhamiria kukijenga kikosi cha Simba vema akiwa na malengo ya kukifikisha mbali pia kwenye mashindano ya kimataifa.

Mbali na wachezaji hao, ilielezwa pia Simba wataendelea kufukuzia saini ya Francis Kahata ambaye walianza kumnyemelea tangu msimu uliopita huku ikielezwa ana majina mengine pia ambayo atahitaji yasajiliwe.

7 COMMENTS:

  1. Tusajiri vizuri, na pia tuombe bahati iwe upande wetu

    ReplyDelete
  2. Huyo jamaa mweusi ni mashine hatari namkumbuks vizuri ni winga wa kushoto anauchezaji wake ni wa aina ya kiprecheche.ana kasi na nguvu alimsumbua sana Yondani na Dante akija ataisaidia sana simba.changamoto ni kwa kina kichuya na Dilunga

    ReplyDelete
  3. Kocha aache tamaa, kikosi cha simba kinajitosheleza kwa msimu huu

    ReplyDelete
  4. Atengeneze mfumo sahihi ili kila mchezaji adumu na kiwango chake kwa muda mrefu la sivyo tutakuwa tunaangamiza fedha zetu bure

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe Yanga...wewe mtu anaweka sawa ubingwa unaleta habari ya kikosi kipo sawa.

      Delete
  5. Huyo guikan hana jipya atakuja kuwa sawa na mohamed rashid, pale Gor mahia alikuwa anakaa benchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by the author.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic