November 6, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Stand United, Bigirimana Blaise raia wa Burundi amesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha kuhakikisha wanaisambaratisha Ruvu Shooting ya Masau Bwire.

Blaise mwenye mabao 4 kwa sasa amesema kuwa kambi yao ambayo wameiweka Mlandizi inawapa uhakika wa kuweza kuchukua pointi tatu.


"Tumejipanga kuweza kupata matokeo kwa kuwa ligi inazidi kushika kasi nasi inabidi tuonyeshe ushindani kwa nini tupo kwenye ligi, tupo tayari kuchukua pointi tatu mbele ya wapinzani wetu," alisema.


Stand United wanashika nafasi ya 12 kwenye ligi baada ya kucheza michezo 13 wakiwa wamejikusanyia pointi 14 watacheza kesho na Ruvu Shooting uwanja wa Mabatini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic