Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amebakiza mkataba wa miezi nane kwenye klabu yake hiyo, uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa haufikirii kwa sasa kumuongezea mkataba mchezaji huyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussen Nyika ameweka wazi kuwa mipango yao kwa sasa ni kuona wanaweza kufanya vizuri kwenye ligi na kuweza kufanyia kazi ripoti ya mwalimu ili wasajili wachezaji wapya.
"Kwa sasa mipango yetu ni kuona timu inafanya vizuri katika mechi zetu za ligi kuu, ripoti ya mwalimu ya kuongeza wachezaji wapya ndio tunaifanyia kazi, ishu ya kuongeza mikataba kwa sasa hatufikirii na siyo Ajibu pekee bali kuna wachezaji wengine wamebakisha miezi sita hadi mitatu," alisema.
Ajibu amehusika katika mabao 11 akitoa pasi nane na kufunga mabao 3 kati ya mabao 19 ya Yanga ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 29.

Mimi kama fan mkubwa was simba nmefurah sana msimamo wa Huyo kocha wa yanga...ajibu ni mchezaji mzuri sana lakini uvivu wake na kujiamini kupita kiasi kwamba hakuna kama yeye ndo sababu kubwa wya kutokukubalika na makocha wanaojua mpira...kuna wachezaji kibao wenye vipaji vikubwa sana lakini bado wanapambana ili wafike mbali,,mpira no kazi na pia ni hatua wachezaji wasipotambua thamani zao....majina yao na vipaji vyao vitayeyuka kama theluji.....hakuna atakayewakumbuka kabisa
ReplyDeleteKikubwa ni kubadilisha aina ya mikataba. Mchezaji ambae anacheza kwa chini ya asilimia kazaa anatakiwa akatwe mshahara. Akifunga zaidi anaongezewa fungu na mambo mengne
ReplyDeleteYanga wanatakiwa kuondoa vimelea vyote vya Simba...wamemtoa Kessy bado huyo Ajib
ReplyDelete