November 8, 2018


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, leo ameondoka kuelekea kwao Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa.

Zahera ameleekea kwao kuipa makali Congo DR ambayo itakuwa inacheza dhidi ya Congo Brazzaville Novemba 18 kuwania tiketi ya kushiriki AFCON 2019.

Licha ya kuondoka, Zahera amesema atarejea mapema kuuwahi mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya mwadui FC utakaopigwa Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Kuelekea mechi hiyo, Zahera amemwamchia maagizo Msaidizi wake, Noel Mwandila kuhakikisha anawafua vizuri vijana wake kwa mechi zijazo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic