December 25, 2018


MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amissi Tambwe amesema kuwa ilimlazimu kusubiri miaka miwili kuweza kufunga mabao matatu 'hat trick' akiwa Yanga jambo ambalo linamfanya azidi kuongeza juhudi kuisaidia timu yake kufikia malengo.

Jana Tambwe aliweka rekodi yake akiwa Yanga baada ya kufikisha hat trick ya saba akiwa Bongo ambapo kati ya hizo tatu alifunga akiwa na Simba ligi kuu msimu wa 2013/14 na tatu nyingine akiwa Yanga msimu wa 2015/16 zote ikiwa ni Ligi kuu, 1 ya kombe la Shirikisho na zote alifunga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tambwe amesema hakuwa na furaha kwa muda mrefu kutokana na kushindwa kufunga hat trick hivyo anaona fahari kuvunja mwiko uliodumu kwa misimu miwili.

"Muda mrefu nilisubiri kuweka rekodi mpya na haikuwa rahisi kufanikiwa kutokana na ushindani, ila nimefanikiwa ni jambo la kushukuru na kuongeza zaidi juhudi kuisaidia timu yangu mpaka kuweza kufanikiwa kuchukua kombe la FA," alisema Tambwe.

Yanga wanafanikiwa kuvuka hatua ya kwanza baada ya kushinda kwa mabao 4-0 mbele ya Tukuyu Stars katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa na kufanya Yanga iendelee kulinda rekodi yake ya kutofungwa kwenye mashidano inayoshiriki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic