December 25, 2018


Uongozi wa Simba umesema unatambua umuhimu wa mashindano ya kombe la Shirikisho, maarufu kama FA hali inayowafanya wachukue tahadhari kubwa watakapocheza kesho na Mashujaa FC ya Kigoma.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema wana kikosi kipana na bora ambacho kina uwezo wa kupata matokeo ila wanaheshimu wapinzani wao Mashujaa katika mchezo wao wa kesho utakaochezwa uwanja wa Taifa.

"Hakuna ambaye hajui ubora wa Simba, tuna kikosi kipana na cha ushindani ila tunawaheshimu wapinzani wetu tunahofia yasije kutokea yale ya Green Warrior, tumewapa tahadhari wachezaji waonyeshe juhudi kutafuta matokeo," alisema.

Msimu wa tatu Simba walitolewa na Green Warrior katika hatua ya kwanza wakiwa ni mabingwa watetezi wa kombe hilo ambalo lipo mikononi mwa Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic