December 27, 2018


KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa ana kazi kubwa ya kuweza kupata matokeo mbele ya kikosi cha Singida United katika mchezo wa Ligi kuu utakaochezwa jumamosi uwanja wa Taifa.

Simba wana pointi 30 wakiwa nafasi ya 13 baada ya kushinda michezo 9 na kupata sare 3 huku wakiwa wamepoteza mchezo 1 kwenye mzunguko wa kwanza.

Aussems amesema kuwa duniani hakuna kocha ambaye anaingia uwanjani akiwa na hesabu za kupoteza mchezo wake hivyo naye ana imani ya kupata ushindi.

"Malengo makubwa na kitu ambacho huwa nawaelekeza wachezaji ni kutafuta pointi tatu uwanjani hali itakayotufanya tuzidi kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye ligi.

"Wachezaji wangu wanauwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo uwanjani hali inayowafanya niwaamini ila tatizo lao ambalo huwa nalifanyia kazi ni safu ya ushambuliaji kukosa umakini wakiwa eneo la hatari, ila tutapambana," alisema.

8 COMMENTS:

  1. Mwandishi nitajie sare 3 za Simba Sc

    ReplyDelete
  2. Mkuu unaitwa Abdallah Simba hata sare mlizotoka huzijui,ulijua kawabambikia nini hehehe

    ReplyDelete
  3. Mwandishi ni bingwa wa kubambika...anatamani simba iwe nafasi ya 13...iko nafasi ya tatu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Atakuwa hajui maana ya herufi P kwenye table(standing)...Namfahamisha kuwa katika msimamo/standings P stands for 'Played' yaani idadi ya michezo iliyocheza. Ahsante

      Delete
  4. Simba sc hawako nafasi ya 13 bali wapo nafasi ya 3

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic