December 21, 2018


Baada ya Kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Taifa, leo watakuwa kibaruani kucheza na Tanzania Prisons utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru.

Ikumbukwe pia KMC walifungwa bao 1-0 na Yanga Taifa na katika mchezo wa Ligi kuu hali inayowafanya waweze kupoteza michezo yao yote kwa vigogo wa Ligi Kuu Tanzania.

Mchezo huu wa leo ni wa Kombe la Shirikisho utapigwa saa 10:00 jioni, utazikutanisha timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, katika mchezo wa Ligi Kuu, KMC walifanikiwa kushinda bao 5-1 walipokutana na Prisons hivyo eo unakuwa ni mtihani wao mpya kwenye kombe la Shirikisho.

Ofisa habari wa KMC, Anwar Binde amesema anatambua ugumu uliopo kwenye ushindani na namna ya kupata matokeo, ila hilo haliwapi taabu kwa kuwa kikosi kina wachezaji wazuri wenye shauku ya kupata matokeo.

"Tumetoka kucheza mchezo mgumu wa Ligi ambapo wapinzani wetu wametushinda, hasira zetu kwa sasa ni mchezo wetu dhidi ya Prisons ambao nao tunajua utakuwa mgumu ila tupo tayari kupambana kupata matokeo," alisema.

Mshindi wa kombe la FA anapata nafasi ya kuwakilisha Taifa katika michuano ya kimataifa ambapo kwa sasa mshindi ni Mtibwa Sugar ambaye kesho atacheza na KCCA ya Uganda, katika mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic