December 22, 2018


Klabu ya Arsenal ya Uingereza inafikiria kufikia makubaliano ya kubadilishana mchezaji wake raia wa Ujerumani, Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 30 na wao kumchukua kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania Isco mwenye umri wa miaka 26. Washika bunduki wa London wako tayari kupokea ofa kutoka kwa klabu nyingine pia (Independent).


Kocha wa klabu ya Leicester City Claude Puel huenda akafutwa kazi wakati wowote baada ya kupoteza uungwaji mkono kutoka kwa wachezaji wake. (Daily Mail).


Basata wanavyoweza kuwazuia Diamond na Rayvanny nje ya TanzaniaKlabu ya Manchester United bado haijakutana na kocha wa zamani wa Real Madrid mfaransa Zinedine Zidane kuhusu uwezekano wa kuwa kocha wao mkuu licha ya kuwepo kwa taarifa tofauti kuhusu nia ya klabu hiyo. (Manchester Evening News).

Klabu ya Sheffield Wednesday inaelezwa kujiandaa kumpa mkataba wa mwaka mmoja kocha wa zamani wa klabu ya Aston Villa Steve Bruce ili achukue nafasi ya kocha Jos Luhukay ambaye alifutwa kazi Ijumaa ya wiki iliyopita. Sheffield Wednesday inataka kumpa mkataba wa paundi milioni 2. (The Sun).

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imeripotiwa kuwa inafikiria uwezekano wa kupata saini ya mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Argentina, Gonzalo Higuain mwenye umri wa miaka 31 kwa kubadilishana na mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata mwenye umri wa miaka 26. (Sky Sports).

Kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri amemuelezea Higuain kama mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa. (ESPN).Kocha Sarri pia anaelezwa kuwa asingependa kumtoa kwa mkopo mwezi ujao kiungo wake raia wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek mwenye umri wa miaka 22. (Guardian).

Kocha wa klabu wa Monaco ya Ufaransa Thierry Henry anataka kumsajili kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ifikapo mwezi Januari. Kiungo huyu wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 anaelezwa kutokuwa na furaha kutokana na kukosa kucheza mechi nyingi msimu huu. (L'Equipe via Daily Mirror).

Kutoka BBC

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic