Nahodha Msaidizi wa kikosi cha Yanga, Juma Abdul amewataka mashabiki kuendelea kuwapa sapoti katika michezo yao inayofuata kutokana na ushindani uliopo na amewatoa wasiwasi juu ya hali ya mlinda mlango Ramadhani Kabwili.
Kabwili aliumia dakika ya 40 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara waliocheza dhidi ya African Lyon uwanja wa Sheikh Amri Abed uliopo Arusha hali iliyofanya awahishwe hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.
"Kikosi kipo sawa na tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya michezo yetu yote ya Ligi Kuu pamoja na ile ya Shirikisho, ushindani ni mkubwa, mashabiki waendelee kutupa sapoti.
"Kabwili yupo sawa na leo alikuwa anafanya mazoezi mepesi tu hivyo dua za mashabiki ni muhimu ili aweze kurejea katika ubora wake na kuendeleza gurudumu la kazi kwenye timu yetu," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment