December 7, 2018


Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mzambia, Clatous Chota Chama, amefunguka machache kuhusiana na moja ya bao alilolifunga dhidi ya Mbabane Swallows katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chama ameandika kuwa hawezi kuchoka kulitazama bao alilofunga huku akimwomba Mungu azidi kuwapa nguvu ya kufuzu pia hatua ijayo.

“Siwezi kuacha kulitazama hili bao asante Mungu kwa kunipa nafasi ya kufunga na kuifanya Simba iweze ku­fanikiwa kwenda hatua nyingine katika michuano hii ya Caf mimi pamoja na wachezaji wenzagu,” alisema Chama.

“Hivyo, basi ninataka kuona timu yangu inafika katika hatua nzuri ya michuano hii mikubwa Afrika na hilo linawezekana kabisa kwa kushirikiana na wen­zangu,” alisema Chama.

Juzi katika mitandao mbalimbali za Zambia gumzo ilikuwa ni Chama huku Nkana wakionywa kuwa nae makini.

Chama tayari ana mabao matatu kwenye Ligi ya Mab­ingwa Afrika huku Bocco na Kagere kila mmoja akiwa na mabao mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic