December 27, 2018


Baada ya kuonesha uzembe katika moja ya mabao aliyofungwa jana kwenye mchezo wa Kombe la FA, mashabiki wa Simba wamemtupia lawama Deogratius Munish 'Dida'.

Simba ilifungwa bao 3-2 na Mashujaa United na kusepeshwa nje ya mashindano hayo huku maana ya kikosi kipana cha Simba kikizua mjadala.

Kutokana na kichapo hicho, baadhi ya mashabiki waliokuwa Uwanjani waliibuka na kusema bao la tatu katika dakika za mwisho ilikuwa ni uzembe wa Dida.

Wapo walioeleza kuwa kipa huyo anajiwekea nafasi ngumu ya kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uzembe ambao aliuonesha kwa kufungwa goli la kirahisi.

Kichapo hicho kimewafanya Simba kuweka rekodi ya aina yake ya kutolewa mara mbili mfululizo kwenye mashindano hayo ikiwa ni baada ya mwaka jana kutolewa na Green Warriors kwa penati.

4 COMMENTS:

  1. mbaya zaidi baada ya kufungwa anacheka mi ningekuwa kocha ningempa benchi akalie mwaka mzima,mshenzi saaaaana huyu

    ReplyDelete
  2. Karibu timu nzima haikuwa timu ya ushindani na kosa kama hilo limekuwa likiendekea kujitokeza. Sijui nani wakulaumiwa, lakini inaumiza sana

    ReplyDelete
  3. Mikia ni mbumbumbu sana!! Hivi wakati mnafanya usajili kwa kuikomoa Yanga mlikuwa hamfikirii yajayo!? Endeleeni kufurahi tu... Bado Wawa ataendelea kuwafurahisha tu...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic