December 7, 2018




Mshambuliaji nyota wa Yanga,Heritier Makambo, mpaka sasa ameweka rekodi ya kibabe ‘konki’ ndani ya kikosi hicho na Ligi Kuu Bara kwa jumla.

Makambo raia wa DR Congo aliyejiunga na Yanga katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu, ameweka rekodi hiyo katika mechi 12 alizocheza za ligi kuu kati ya 14 ambazo timu yake imecheza mpaka sasa.

Rekodi aliyoiweka Mkongomani huyo ni ile ya mabao aliyofunga baada ya hadi sasa kufunga mabao saba sawa na Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wa Simba.

Ipo hivi; Makambo mabao yake yote saba ameyafunga katika kipindi cha kwanza. Hakuna mchezaji mwingine mwenye mabao mengi kama yeye au zaidi ambaye amefanya hivyo.

Pia katika mechi zote alizofunga mabao hayo, yeye ndiye anakuwa mchezaji wa kwanza kwenye mechi husika kuanza kucheka na nyavu. Hakuna mwingine aliyefanya hivyo.

Mechi alizofunga ni hizi; Yanga 2-1 Mtibwa (Makambo dk 31, Kelvin Yondani 4. La Mtibwa ni Haruna Chanongo dk 73). Yanga 1-0 Coastal (Makambo dk 11). Yanga 3-0 Alliance (Makambo 18, Mrisho Ngassa dk 25, Ibrahim Ajibu dk 86). Yanga 1-0 Lipuli (Makambo dk 10).

Mwadui 1-2 Yanga (Makambo dk 10, Ngassa 59. Mwadui mfungaji Salim Aiyee dk 40). Kagera 1-2 Yanga (Makambo dk 21, Raphael Daud dk 74. Kagera mfungaji Ramadhan Kapera dk 32) na Yanga 3-0 JKT Tanzania ( Makambo dk 20, Ngassa dk 53 na Ajibu dk 79).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic