December 31, 2018


Nahodha wa Simba, John Bocco, ameweka wazi licha ya kupangwa na timu mbili kutoka mataifa ya Uarabuni katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wamejipanga kuweka rekodi kuhakikisha wanawafunga kila watakapokutana nao na kusonga mbele katika hatua hiyo.

Bocco ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosaidia kikosi hicho kutinga hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika ambapo wamepangwa katika Kundi D. Kundi hilo lina timu za Al Ahly ya Misri, JS Saoura ya Algeria pamoja na AS Vita ya DR Congo huku mechi yao ya kwanza ya hatua hiyo wakitarajia kucheza Januari 11 mwakani.

Bocco ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wameona kundi ambalo wamepangwa na tayari wameanza kujiandaa kikamilifu kuhakikisha wanazifunga timu zote ambazo watacheza nazo katika Uwanja wa Taifa zikiwemo Al Ahly na JS Saoura.

“Mashindano haya ni magumu na kundi tayari tumeliona, kwetu hili ni kundi zuri na tutapambana kwa ajili ya kusonga mbele katika kundi kwa kushika nafasi za juu. “Watu wamekuwa wakiona tukipoteza mara nyingi mbele ya timu za Kiarabu lakini kwa msimu huu niwaambie kwamba tutaweka historia kwa kuwachapa wote ambao tutacheza nao.

“Sisi hatuchezi kwa historia eti kwamba tulipoteza mechi na timu fulani bali tunacheza kwa kilichopo mbele yetu, kwa hiyo naamini tutajipanga vizuri kwa msimu huu na lengo letu ni kuweka rekodi,” alisema Bocco.

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Bocco aongeze umakini kurudisha makali yake ya msimu uliopita. Kwa ukongwe wake kwenye ligi akiweza kutatua changamoto alizonazo sasa za kupoteza nafasi nzuri za kufunga atakua somo zuri sana kwa young strikers.

    ReplyDelete
  2. Kabisa BOKO ana nafasi ya kuisaidia Simba kwenye mashindano haya klabu bingwa Africa ila ajirekebishe sana. Watanzania wangefurahi kumuona Boko aliyemakini na msumbufu asiepoteza nafasi za wazi hovyo na mwenye kujali zaidi ushirikiano wa hali ya juu katika safu ya umaliziaji kwani ni pacha wa Samata pia kwenye timu ya taifa .Boko amepata bahati ya kuaminiwa na kocha wake mkuu pale Simba lakini inaonesha yeye mwenyewe Boko amepoteza kujiamini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic