December 26, 2018


Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 unatara­jia kufikia tamati hivi karibuni baada ya timu zote 20, kucheza mechi 19 ambapo kwa sasa ipo raundi ya 17 kwa baadhi ya mechi huku nyingine zikiwa chini ya hapo.

Licha ya ligi kufikia hatua hiyo, timu mbalimbali zimekuwa zikionyesha uwezo wa hali ya juu huku Bodi ya Ligi Tanzania imekuwa ikitoa tuzo kwa wachezaji na mako­cha waliofanya vyema katika mechi mbalimbali ikiwa ni zoezi endelevu hadi mwisho wa msimu kwa kila mwezi.

Championi Jumatano, linakucha­mbulia wachezaji na makocha ambao wameanza kupata tuzo hizo tangu ligi hiyo ianze kutimua vumbi Agosti 22.

MEDDIE KAGERE, AGOSTI

Mshambuliaji wa Simba raia wa Rwanda, amekuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti, ame­pata tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji Joseph Mahundi wa Azam FC na Omary Mponda wa Kagera Sugar.

Kagere alifanikiwa kupata nafasi hiyo, baada ya kutoa mchango mkubwa kwa kuisaidia timu yake kupata pointi sita na kushika nafasi ya tatu katika msi­mamo wa ligi, akifunga mabao matatu ambapo la kwanza alifunga dhidi ya Tanzania Prisons katika ushindi wa bao 1-0 na mawili alifunga mchezo dhidi ya Mbeya City katika ushindi wa mabao 2-0.

AMRI SAID, AGOSTI

Baada ya bodi ya ligi kuona umuhimu wa kuteua wachezaji bora wa mwezi, imeamua kuwa na tuzo ya makocha bora ambapo kwa mara ya kwanza kuanza kutolewa mwezi Agosti, kocha wa Mbao FC, Amri Saidi alitangazwa kuwa kocha bora kutokana na timu yake kufanya vizuri.

ELIUD AMBOKILE, SEPTEMBA

Mshambuliaji wa Mbeya City ya mko­a n i Mbeya, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba, alitwaa tuzo hiyo baa­da ya kuwashinda wa­shambuliaji, Ibrahim Ajibu wa Yanga na Sta­mili Mbonde wa Mtibwa Sugar.

Ambokile ametwaa tuzo hiyo baada ya ku­funga mabao manne, wakati Mbeya City ikishinda michezo miwili, sare moja na kupoteza michezo miwili.

MWINYI ZAHERA, SEPTEMBA, NOVEMBA

Alichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu Bara mwezi Sep­temba baada ya kuwapiku makocha Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar na Bakari Shime wa JKT Tanzania baada ya timu yake kufanya vizuri ka­tika mwezi huo.

Pia, kocha huyo amefanikiwa kuwa kocha bora wa mwezi Novemba kuto­kana na kuisimamia timu yake hiyo kufanya vizuri kwa kupata pointi 10 kwa kushinda michezo mitatu na ku­toa sare mmoja hivyo kuongoza msi­mamo wa ligi.

Aliwabwaga makocha Juma Mgunda wa Coastal Union na Kaimu Kocha Mkuu wa Alliance FC, Gilbert Dadi alioingia nao hatua ya mwisho.

EMANNUEL OKWI, OKTOBA

M s h a m ­buliaji wa Simba, Em­m a n u e l O k w i raia wa Ug anda a l i fa ni­kiwa ku­chukua tuzo ya u c h e zaji bora wa mwezi Oktoba baada ya kuwapiku washambuliaji Eliud Ambokile wa Mbeya City na Yahya Zayd wa Azam FC.

Okwi alitwaa tuzo hiyo, baada ya kuisaidia timu yake kutwaa pointi 12 katika mechi nne ilizo­cheza mwezi Oktoba kwa kushin­da mechi zote na kuifanya timu yake kumaliza ikiwa nafasi ya pili huku akifanikiwa kufunga mabao saba ikiwa ni pamoja na ‘hat trick’ aliyoifunga katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting katika ushindi wa mabao 5-0.

HANS PLUIJM, OKTOBA

Alichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Oktoba baada ya kuiongoza Azam kupata pointi 15 baada ya kushinda michezo yote mitano iliyocheza na kushika nafasi ya kwanza huku akiwatupa mbali kocha wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ra­madhan Nsuzwarimo.

Aussems akiiongoza Simba kushinda michezo yote minne iliyocheza hivyo kupata pointi 12 na kushika nafasi ya pili, wakati Nsuzwarimo alipata pointi 11 akishinda michezo mitatu na kutoka sare mbili akiiwezesha timu yake kupan­da hadi nafasi ya nane.

HERITIER MAKAMBO, NOVEMBA

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ wa Yanga al­iokuwa anagombea nao.

Amepata tuzo hiyo kufuatia timu yake ya Yanga kufanya vizuri katika michezo minne, ambapo Makambo al­itoa mchango mkubwa kwa timu yake hiyo kupata pointi 10 kwa kushinda michezo mitatu na kutoka sare moja ikiwa nafasi ya kwanza, ambapo mshambuliaji huyo alifunga mabao matatu.

Shaibu alitoa mchango wake katika safu ya ulinzi katika timu yake hiyo, hivyo kuifanya timu yake hiyo kuwa moja ya timu yenye ngome imara ka­tika ligi na kwa upande wa Dilunga mchango mkubwa kwa Ruvu Shooting akifunga mabao matatu katika mich­ezo mitatu ambayo timu yake ilicheza ikishinda mmoja na kupoteza miwili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic