December 26, 2018


MASHINDANO ya Mapinduzi Cup yanatarajiwa kuanza Januari Mosi na kumalizika Januari 13 yakihusisha timu 9 ambazo zitagombania ubingwa ulio mikononi mwa Azam FC.

Timu Kutoka nje ya Tanzania zimekwama kushiriki mashindano kwa kueleza kuwa ni kubwana na ratiba ya Ligi zao kwa timu ya Bandari ya Kenya pamoja na URA ya Uganda URA.

Mabingwa watetezi Azam FC watashuka dimbani Januari 2 kuvaana na Jamhuri, huku Ya nga watashuka dimbani Januari 03 kuvaana na KVS wakati Simba wao Januari 4 watamenyana na Chipukizi.

Kombe hilo lina makundi mawili ambayo yana timu 4 isipokuwa kundi B lina timu tano ambazo zinashiriki, Kundi A lina timu kama Chipukizi, Mlandenge, KMKM na Simba huku B likiwa na timu 5 ambazo ni KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.

Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo imesema kuwa Zawadi kwa mshindi wa kwanza itaongezwa kutoka milioni 10 mpaka milioni 15 ikiwa ni pamoja na medali za dhahabu pamoja na kombe na mashindano hayo yatatumia uwanja wa Amaan kwa mechi zote mpaka nusu Fainali na Uwanja wa Gombani kwa mechi ya Fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic