December 6, 2018



Baada ya Simba kutinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kibabe, wamechekelea kupangwa na Nkana FC ya Zambia kwa kuwa ni timu bora.

Nkana FC ambayo Mtanzania Hassan Kessy aliyeitumikia timu ya Simba anaichezea kwa sasa, pia ni nyumbani kwa nyota Clatous Chama ambaye pia anachezea timu ya Taifa ya Zambia.


Beki kiraka wa Simba, Erasto Nyoni, amesema wanaamini ni timu nzuri watakayokutana nayo kwenye hatua hiyo ya kwanza ila hesabu zao ni kuweza kupata matokeo na kusonga mbele.


"Nkana ni timu bora na ndio maana imeweza kupata matokeo, hivyo tunajua kilicho mbele yetu kwa kuwa tunaiwakilisha nchi yetu, tutahakikisha tunaipeperusha bendera kwa manufaa ya Taifa letu," alisema.


Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 14 au 16 nchini Zambia na mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 21 au 23 uwanja wa Taifa.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic