December 6, 2018


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amesema bado ana kazi kubwa ya kuhakikisha anaisaidia timu yake kupata matokeo katika michezo yote ya ligi kuu ili kuweza kujiweka kwenye mazingira mazuri ndani ya ligi.


Ajibu ambaye kwa sasa amefikisha jumla ya mabao 5 kwenye Ligi Kuu na ametengeneza jumla ya pasi 9 za mwisho za mabao kati ya 27 waliyofunga Yanga ambao ni vinara wa Ligi kuu kwa sasa wakiwa na pointi 38.


Ajibu amesema bado kuna kazi nzito ya kufanya hasa kutokana na kupata matokeo mazuri kwa timu yao hawapaswi kubetweka bali kuongeza zaidi juhudi.

"Kazi bado inaanza kwa sasa kwa kuwa kuna michezo mingi ambayo ipo mbele yetu hivyo tunakazi ya pamoja kuhakikisha tunafanikiwa kufikia malengo yetu ambayo tumejiwekea ili tuendelee kufanya vizuri zaidi.


"Wachezaji wengi ambao tupo nao kila mmoja ana tabia zake na pia wengine hawajawa kwenye ligi muda mrefu sasa ili kuweza kuwekana sawa ni lazima tuendelee kuelekezana hata tukiwa ndani ya uwanja tusiendelee kukosea, makosa yapo ila tunapaswa tuelekezane," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic